Advertisements

Tuesday, April 23, 2024

PSPTB YATOA ELIMU CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR

 

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi akitoa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Afisa TEHAMA kutoka PSPTB Elihuruma Eliufoo akitoa mada kuhusu namna ya mwanafunzi anavyoweza kujisajili pamoja na kufanya mitihani ya Bodi wakati wa kutoa elimu kwa wa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Afisa Ununuzi kutoka Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), AllyYassin Mbarouk akitoa maelezo kuhusu namna ya kuongeza dhamani kwenye taaluma hiyo kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

DKT. DIMWA : AJIVUNIA HAZINA YA WAZEE WA CCM


NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, akizungumza na kada wa CCM ndugu Waalidi Psinarie Kavishe(wa kwanza kushoto) nyumbani kwake Kwa mchina mwanzo Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa(upande wa kulia),akizungumza na Kadhi Mkuu mstaafu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis nyumbani kwake Mwanakwerekwe Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba mstaafu ndugu Salum Juma Tindwa nyumbani kwake kwa Mchina Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, akizungumza na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Wanawake na Watoto Zanzibar ndugu Msham Abdallah Khamis nyumbani kwake Chuini Unguja.

ZANZIBAR YAUNGANA NA DUNIA KUADHIMISHA KILELE CHA WIKI YA MAABARA DUNIANI


Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akikata utepe kuashiria uzinduzi wa sera ya maabara Zanzibar katika kilele cha wiki ya maabara iliyofanyika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.

Na Fauzia Mussa, Maelezo
Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka wataalamu wa Maabara kuvifanyia utafiti vitu wanavyovichunguza ikiwemo maradhi ili kuyadhibiti kwa njia za kisayansi.

Akisoma hotuba ya Rais Mwinyi katika kilele cha wiki ya Maabara Duniani huko Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar alipomwakilisha, Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kufanya hivyo kutasaidia taasisi kudhibiti maradhi na kuzielekeza njia zinazoshauriwa kirahisi kutokana na kuwepo na ushahidi wa Kisayansi.

Aidha amewataka wataalamu hao kuongeza nguvu kwenye Taasisi za Tafiti ikiwemo za Taaisi ya Afya ya Binaadamu (ZAHRI), Utafiti wa Mifugo (ZALIRI), Taasisi ya Utafiti wa Safayansi ya Baharini (ZAFIRI) ili kuweza kufikia malengo yaliokusudiwa.

Amefahamisha kuwa Maabara zote zina mchango mkubwa kwa maendeleo mbalimbali ikiwemo ya afya na huduma zinazotolewa kwa wananchi, hivyo Serikali itaendelea kuimarisha Maabara zote ili kuweza kuendeleza kazi za uchunguzi wa maradhi, vinasaba, kemikali, pamoja na vyakula.

RAIS WA DK.HUSSEIN MWINYI AMEJUMUIKA NA WANAVYUONI NA MASHEIKH KATIKA HAULI NA DUA YA KUMUOMBEA MAREHEMU ALHABYB AHMAD BIN ABUUBKAR SUMEIT



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya kumuombea marehemu Mwanachuoni Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit ikisomwa na Sayy Mudh-hiridin Ally Qullatein (kushoto kwa Rais) wakiwa katika kaburi la marehemu lililoko katika eneo la Msikiti wa Ijumaa Malindi Wilaya Mjini Unguja, wakati wa hafla ya Hauli ya 102 iliyofanyika leo 22-4-2024 na (kushoto kwake) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Masheikh na Wananchi mbalimbali katika Kisomo cha Hauli ya 102 ya kumuombe Marehemu Mwanachuoni Mkubwa Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit, iliyofanyika leo 22-4-2024 katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Sheikh. Sayy Mudh-hiridin Ally Qullatein


SAYY.Omar Bin Ally Qullatein akihitimisha kisomo cha Hauli ya 102 ya kumuombea Marehemu Mwanachuoni Mkubwa Zanzibar Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit, iliyofanyika leo 22-4-2024 katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, na (kushoto kwake) Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume

Sunday, April 21, 2024

WAZIRI MKUU AWAAGA VIONGOZI WA DINI, UZINDUZI WA ROUTE YA SGR DAR - DODOMA

L
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaaga viongozi wa dini 104 ambao wanaelekea Dodoma kwa treni ya mwendokasi (SGR) kwenda kushiriki ibada maalum ya kuliombea Taifa inayotarajiwa kufanyika kesho, Jumatatu, Aprili 22, 2024.

Treni hiyo imeondoka stesheni ya Dar es Salaam saa 8.53 mchana ikiwa na viongozi hao, waandishi wa habari, waimbaji wa nyimbo za injili na kaswida, viongozi wastaafu wa Serikali, watendaji wa Shirika la Reli nchini, wawakilishi wa ubalozi na watedaji wengine wa Serikali.
Amewaaga viongozi hao na watendaji wengine wa Serikali na taasisi mbalimbali leo (Jumapili, Aprili 21, 2024) kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye stesheni ya Tanzanite, barabara ya Sokoine, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na viongozi hao kabla ya kupata dua ya kuombea safari yao, Waziri Mkuu amesema: “Leo ni siku muhimu na ya kihistoria kwa nchi yetu. Tuko kwenye wiki ya maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano na tunashuhudia safari ya kwanza ya treni ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.”

MABALOZI WA TANZANIA WAJIFINGIA KIBAHA, KUTAFAKARI NA KUJIPANGA UPYA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na Mabalozi kuelekea warsha inayotarajiwa kuanza tarehe 21 Aprili 2024 mjini Kibaha, Pwani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza kwenye kikao kazi kuelekea warsha ya Mabalozi inayotarajiwa kuanza tarehe 21 Aprili 2024 mjini Kibaha, Pwani
Sehemu ya Mabalozi wakifurahia jambo wakati Waziri Makamba akizungumza kwenye kikao cha maandalizi kuelekea warsha ya Mabalozi inayotarajiwa kuanza tarehe 21 Aprili 2024 mjini Kibaha, Pwani
Mwenyekiti wa Umoja wa Mabalozi Wastaafu Mhe. Balozi Aziz Ponary Mlima akizungumza kwenye kikao cha maandalizi kuelekea warsha ya Mabalozi inayotarajiwa kuanza tarehe 21 Aprili 2024 mjini Kibaha, Pwani

WAZIRI MKUU AAGIZA TAARIFA MAALUM YA UDHIBITI WA UVUVI HARAMU


*Azindua boti ya doria kukabiliana na uhalifu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza taarifa maalum ya udhibiti wa vitendo vya uvuvi haramu iwasilishwe kabla ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi haijawasilisha hotuba ya bajeti ya mwaka 2024/2025.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Aprili 21, 2024) katika hafla ya uzinduzi wa boti maalum kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika bahari hapa nchini iliyofanyika bandarini jijini Dar es Salaam.

“Taarifa kuhusiana na shughuli maalum ya udhibiti wa vitendo vya uvuvi haramu katika ukanda wa Bahari kuu iwasilishwe kabla ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi haijawasilisha hotuba ya bajeti ya mwaka 2024/2025,” amesema.

Ameishukuru Serikali ya Japan kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha mipango ya maendeleo ambayo imechangia dola za Marekani 500,000 kwenye ununuzi wa boti hiyo. “Ninaiomba Serikali ya Japan isichoke kutusaidia ili tuweze kukamilisha utekelezaji wa mikakati iliyopo katika eneo hili la kukabiliana na uhalifu nchini,” amesema.

Saturday, April 20, 2024

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR KUENDESHA ZOEZI LA CHANJO YA SHINGO LA KIZAZI


Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fatma Kabole akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na zoezi la chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana kati ya umri wa miaka 9-14, inayotarajiwa kuanza April 22-25 nchi mzima, hafla ambayo imefanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Unguja.

Na Fuzia Mussa. Maelezo Zanzibar.
Wizara ya Afya Zanzibar inatarajia kuendesha zoezi la chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa wasichana wenye umri kati ya miaka 9 -14 ili kuwalinda na ugonjwa huo.

Akizungumza na Waandishi wa habari huko Wizara ya Afya Mnazimmoja Wilaya ya Mjini, Naibu Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fatma Kabole amesema zoezi hilo linatarajia kuwafikia watoto zaidi ya laki moja katika Skuli za Serikali na binafsi

Aidha amefahamisha kuwa kumewekwa utaratibu maalum wa kuwafikia watoto walioko majumbani kupitia wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ili kuweza kupata chanjo hiyo.

Amesema taakwimu zinaonesha kuwa saratani ya mlango wa kizazi inaongoza kuathiri wananwake ambapo kiasi ya wananwake 466,000 wanagundulika na tatizo hilo kila mwaka wengi wao wanatoka nchi zinazoendelea ikiwemo Zanzibar.

RAIS DK.HUSSEIN ALI MWINYI AZINDUA TAASISI YA WASANIFU,WAHANDISI NA WAKADIRIAJI MAJENGO


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi, alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar, Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya Uzinduzi wa Taasisi ya Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji, uliofanyika leo 20-4-2024 katika ukumbi wa Hoteli hiyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Afisa Masoko wa Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC)Ndg.Nurdin Hussein Mohamed,wakati akitembelea maonesho katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji, uliyofanyika leo 20-4-2024, katika ukumbi wa hoteli hiyo na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji na (kulia kwa Rais) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya PADDCO Ndg. Afla Abdalla Mrusi,wakati akitembelea maonesho ya Wahandisi katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar, kabla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji, uliyofanyika leo 20-4-2024, katika ukumbi wa hoteli hiyo na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Mohamed Salum na (kulia kwa Rais) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya Al Hatmy Desigh&Engineering Consultancy Zanzibar Ndg.Abdulhamid Mohammed Ali Mhoma akitowa maelezo ya michoro ya majengo inayojenga kampuni hiyo Zanzibar,wakati akitembelea maonesho ya Wahandisi katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar, kabla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji, uliyofanyika leo 20-4-2024, katika ukumbi wa hoteli hiyo na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Mohamed Salum na (kulia kwa Rais) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja. Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMTAKIA HERI YA KUMBUKUMBU YA SIKU YA KUZALIWA MZEE MALECELA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela zawadi ya kikombe alipokwenda nyumbani kwa Mheshimiwa Malecela eneo la Uzunguni jijini Dodoma kumtakia heri ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa , Aprili 19, 2024. Katikati ni mke wa Mzee Malecela Ambaye pia ni Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela zawadi alipokwenda nyumbani kwa Mheshimiwa Malecela eneo la Uzunguni jijini Dodoma kumtakia heri ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, Aprili 19, 2024.Katikati ni mke wa Mzee Malecela Ambaye pia ni Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela alipokwenda nyumbani kwa Mheshimiwa Malecela eneo la Uzunguni jijini Dodoma kumtakia heri ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, Aprili 19, 2024. Kulia ni mke wa Mzee Malecela Ambaye pia ni Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKAGUZI MKUU WA NDANI KUONGEZA USIMAMIZI WA MAPATO NA MATUMIZI


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, akitoa mafunzo ya Afya yanayomwezesha mkaguzi wa ndani kufanya kazi zake kwa ufanisi, wakati wa Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Mkaguzi wa Ndani katika nchi 27 Afrika wakiwa katika Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) ulioangazia taratibu za ukaguzi wa ndani, utawala bora na mazingira, uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Na. Peter Haule, WF. Arusha
Mkaguzi Mkuu wa Ndani (IAG), Bw. Benjamini Magai amesema ofisi yake itafanya mabadiliko makubwa katika taratibu za ukaguzi katika maeneo ya mapato na matumizi kutokana na mafunzo muhimu waliyoyapata katika Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA)

Hayo aliyasema jijini Arusha wakati wa kuhitimisha siku tano za Mkutano wa 10 wa Shirikisho hilo uliowakutanisha zaidi ya wajumbe 1200 kutoka nchi 27 za Afrika na nje ya Afrika.

KATIBU TAWALA SAME AONGOZA UPANDAJI MITI KUELEKEA KUSHEREHEKEA MIAKA 60 YA MUUNGANO



KATIBU Tawala wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Upendo Wella amesema katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanikiwa kusimamia masuala ya muungano kwa ufanisi mkubwa.

Hiyo imesababisha kuimarika kwa utaifa, umoja, amani, utulivu, na hali ya maisha ya wananchi kutokana na ukuaji wa uchumi wa pande zote mbili za Muungano.

Wella ametoa kauli hiyo alipowaongoza wananchi katika upandaji miti ikiwa ni shamshara za sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Zoezi hilo lilifanyika leo katika Kata ya Kisima, wilayani Same.

Aidha,amewahimiza wananchi wa wilaya ya Same kuendeleza utamaduni wa kupanda miti sehemu mbalimbali, hasa kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha kwa wingi, ili miti iweze kustawi vyema na kuepukana na hali ya ukame.

RAIS DKT. MWINYI AFUNGUA MSIKITI WA MASJID AL ABRAAR


MUONEKANO wa Masjid Al Abraar Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, na kujumuika na Wananchi wa Kijiji cha Tazari katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo 19-4-2024 katika Masjid hiyo
SHEHA wa Shehia ya Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja akizungumza na kutowa shukrani za Wananchi wa Kijiji cha Tazari, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari Mkoa wa Kaskazini Unguja 19-4-2024, wakati wa ufunguzi wa Msikiti huo uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi na kujumuika katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.
MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wananchi kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi wa Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja 19-4-02024, katika hafla ya ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Tazari baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja uliyofanyika 19-4-2024

KONGAMANO LA MIAKA 60 LINATARAJIWA KUFANYIKA TUNGUU ZANZIBAR


Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (Centre Foreign Relation) Dkt. Jacob G. Nduye (Kushoto) akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kususiana na Kongamano la Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar litakalofanyika tarehe 30 Aprili, 2024, katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohammed Shein Tunguu Zanzibar.

Na Ali Issa. Maelezo Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussen Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la siku moja la miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, linalotarajiwa kufanyika tarehe 30 mwezi huu katika ukumbi wa Dkt. Shein Tunguu Wilaya ya Kati.

Kongamano hilo litafanyika kwa ushirikiano wa Chuo cha Utawala wa Uma Zanzibar (IPA) na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim kilichopo jijini Dar-es-salaam.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari huko Chuo cha Utawala wa Uma Tunguu Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, Dkt. Jacob Nduye amesema mjadala huo utafanyika ili kuleta uelewa, ufafanuzi na historia ya safari ya miaka 60 tangu kuasisiwa kwake.

Amesema pia kutakuwa na uchambuzi wa viongozi waliopita kwa awamu nane madarakani kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa awamu ya sita.

TUNAHITAJI KUWA NA JENGO KUBWA NA LA KISASA KAMA HILI LENYE VIFAA NA UWEZO WA KUHUDUMIA ONGEZEKO LA WAGENI WANAOKUJA NCHINI - DKT. MWINYI


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema huduma za uhamiaji kwa Mkoa wa Mjini Magharibi zinahitaji kuwekewa mazingatio maalumu ya kuimarishwa wake.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Ofisi za Jeshi la Uhamiaji kwa Mkoa wa Mjini Magharibi, maeneo ya Mazizini Wilaya ya Mjini.

Alisema, Mkoa huo una vituo vya uingiaji na utokaji wa watu vikiwemo, bandari ya Malindi ambayo kwa mwaka hupokea zaidi ya watalii wa Kimataifa 20,000 na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume pia hupokea zaidi ya watalii 500,000 kwa mwaka.

“Tunahitaji kuwa na jengo kubwa na la kisasa kama hili, lenye vifaa na uwezo wa kuhudumia ongezeko la wageni wanaokuja nchini kwa dhamira tofauti ikiwemo uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za Uchumi”. Alifafanua Rais Dk. Mwinyi.

Alisema, kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo kutaongeza na kuimarisha ari na kasi ya utoaji wa huduma bora za Uhamiaji, kwa Mkoa wa Mjini Magharibi na Manispaa zake tatu.

TANZIA: MTANGAZAJI WA CLOUDS FM GADNER G.HABASH AFARIKI DUNIA



Mtangazaji Mahiri wa Clouds FM, Gadner G. Habash (50) amefariki Dunia Leo April 20, 2024.

Gadner maarufu kama ‘Captain’ aliejizolea Umaarufu Mkubwa kupitia Kipindi cha Jahazi, alikua amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa na Pressure (Shinikizo la Damu).

Vijimambo Blog Tunatoa Pole kwa Familia , Clouds Media Group , Ndugu Jamaa na Marafiki . Mungu ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi Amein

Friday, April 19, 2024

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KATIKA JUKWAA LA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA NA UTURUKI JIJINI ISTANBUL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyabiashara na Wawekezaji katika Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki lililofanyika Jijini Istanbul tarehe 19 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Uturuki Mhe. Cevdet Yilmaz pamoja na viongozi mbalimbali katika Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki lililofanyika Jijini Istanbul tarehe 19 Aprili, 2024.
Makamu wa Rais wa Uturuki Mhe. Cevdet Yilmaz akizungumza katika Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki lililofanyika Jijini Istanbul tarehe 19 Aprili, 2024.

WAONGOZA NDEGE KUTOKA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA YA UGANDA (UCAA) WAHITIMU KATIKA CHA CATC


Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akizungumza na wahitimu wa  mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akizungumza jambo pamoja kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akiwakabidhi vyeti pamoja na zawadi kwa  wahitimu wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)